Naye Hilkia, kuhani mkuu, akamwambia Shafani, mwandishi, Nimekiona kitabu cha torati katika nyumba ya BWANA. Hilkia akampa Shafani kile kitabu, naye akakisoma.