1 Tim. 4:7-13 Swahili Union Version (SUV)

7. Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa.

8. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.

9. Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa;

10. kwa maana twajitaabisha na kujitahidi kwa kusudi hili, kwa sababu tunamtumaini Mungu aliye hai, aliye Mwokozi wa watu wote, hasa wa waaminio.

11. Mambo hayo uyaagize na kuyafundisha.

12. Mtu awaye yote asiudharau ujana wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo, na katika upendo na imani na usafi.

13. Hata nitakapokuja, ufanye bidii katika kusoma na kuonya na kufundisha.

1 Tim. 4