8. Vivyo hivyo mashemasi8 na wawe wastahivu; si wenye kauli mbili, si watu wa kutumia mvinyo sana, si watu wanaotamani fedha ya aibu;
9. wakiishika siri ya imani katika dhamiri safi.
10. Hawa pia na wajaribiwe kwanza; baadaye waitende kazi ya shemasi, wakiisha kuonekana kuwa hawana hatia.
11. Vivyo hivyo wake zao na wawe wastahivu; si wasingiziaji; watu wa kiasi, waaminifu katika mambo yote.
12. Mashemasi na wawe waume wa mke mmoja, wakiwasimamia watoto wao vizuri, na nyumba zao.
13. Kwa maana watendao vema kazi ya shemasi hujipatia daraja nzuri, na ujasiri mwingi katika imani iliyo katika Kristo Yesu.
14. Nakuandikia hayo nikitaraji kuja kwako hivi karibu.
15. Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli.
16. Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu.Mungu alidhihirishwa katika mwili,Akajulika kuwa na haki katika roho,Akaonekana na malaika,Akahubiriwa katika mataifa,Akaaminiwa katika ulimwengu,Akachukuliwa juu katika utukufu.