2. Nao mashehe wa Wafilisti wakapita mbele, mia kwa mia, na elfu kwa elfu; naye Daudi na watu wake wakapita wa mwisho pamoja na Akishi.
3. Ndipo wakuu wa Wafilisti wakasema, Waebrania hawa wafanyani hapa? Naye Akishi akawaambia wakuu wa Wafilisti, Je! Siye huyu Daudi, yule mtumishi wa Sauli, mfalme wa Israeli, ambaye amefuatana na mimi siku hizi, naam, miaka hii, wala mimi nisione hatia kwake, tangu hapo aliponiangukia mimi hata leo?
4. Lakini wakuu wa Wafilisti wakamkasirikia; nao wakuu wa Wafilisti wakamwambia, Mrudishe huyu, apate kurejea mahali pake ulipomwagiza, wala asiende pamoja nasi vitani, asije akawa adui wetu vitani; kwani mtu huyu angejipatanisha na bwana wake kwa njia gani? Je! Si kwa vichwa vya watu hawa?