4. mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana.
5. Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.
6. Maana kwa ajili hiyo hata hao waliokufa walihubiriwa Injili, ili kwamba wahukumiwe katika mwili kama wahukumiwavyo wanadamu; bali wawe hai katika roho kama Mungu alivyo hai.
7. Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na akili, mkeshe katika sala.
8. Zaidi ya yote iweni na juhudi nyingi katika kupendana; kwa sababu upendano husitiri wingi wa dhambi.