1. Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
2. Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
3. ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.
4. Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
5. Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa mwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
6. Kwa kuwa imeandikwa katika maandikoTazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima,Na kila amwaminiye hatatahayarika.