28. Na baadhi yao walikuwa na ulinzi wa vyombo vya huduma; kwani huingizwa kwa hesabu, na kutolewa kwa hesabu vile vile.
29. Na baadhi yao waliamaniwa kuviangalia vyombo vya nyumbani, na vyombo vyote vya Patakatifu; na kuwa juu ya unga safi, na divai, na mafuta, na ubani, na manukato.
30. Na baadhi ya wana wa makuhani waliweka tayari machanganyiko ya manukato.
31. Naye Matithia, Mlawi mmojawapo, aliyekuwa mzaliwa wa kwanza wa Shalumu, Mkora, aliamaniwa kazi ya kuviangalia vitu vile vilivyookwa kaangoni.
32. Na baadhi ya ndugu zao, wa wana wa Wakohathi, walikuwa juu ya mikate ile ya Wonyesho, ili kuiandaa kila sabato.
33. Tena hawa ndio waimbaji, wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, ambao walikaa vyumbani, kisha walikuwa hawana kazi nyingine; kwa kuwa walitumika katika kazi yao mchana na usiku.
34. Hao walikuwa wakuu wa mbari za baba zao katika Walawi, katika vizazi vyao vyote, watu wakuu; nao walikuwa wakikaa huko Yerusalemu.
35. Basi huko Gibea alikaa babaye Gibea, jina lake Yeieli, na jina la mkewe aliitwa Maaka;
36. na mwanawe, mzaliwa wake wa kwanza, alikuwa Abdoni; na Suri, na Kishi, na Baali, na Meri, na Nadabu;
37. na Gedori, na Ahio, na Zekaria, na Miklothi.
38. Na Miklothi akamzaa Shimea. Hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao.
39. Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.