32. Na Miklothi akamzaa Shimea. Na hao nao walikuwa wakikaa pamoja na ndugu zao huko Yerusalemu, kuwakabili ndugu zao.
33. Naye Neri akamzaa Kishi; na Kishi akamzaa Sauli; na Sauli akamzaa Yonathani, na Malkishua, na Abinadabu, na Eshbaali.
34. Na mwanawe Yonathani alikuwa Meribaali; na Meribaali akamzaa Mika.
35. Na wana wa Mika; Pithoni, na Meleki, na Tarea, na Ahazi.
36. Na Ahazi akamzaa Yara; na Yara akamzaa Alemethi, na Azmawethi, na Zimri; na Zimri akamzaa Mosa;
37. na Mosa akamzaa Binea; na mwanawe huyo alikuwa Refaya, na mwanawe huyo ni Ekasa, na mwanawe huyo ni Aseli;
38. naye Aseli alikuwa na wana sita, ambao majina yao ni haya; Azrikamu, na Bokeru, na Ishmaeli, na Shearia, na Obadia, na Hanani. Hao wote walikuwa wana wa Aseli.
39. Na wana wa Esheki nduguye ni hawa; mzaliwa wake wa kwanza, Ulamu, na wa pili Yeushi, na wa tatu Elifeleti.
40. Na wana wa Ulamu walikuwa watu hodari wa vita, wapiga upinde, nao walikuwa na wana wengi, na wana wa wana, watu mia na hamsini. Hao wote ndio waliokuwa wana wa Benyamini.