1 Nya. 7:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni, wanne.

2. Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa mbari za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu ishirini na mbili elfu na mia sita.

3. Na wana wa Uzi; Izrahia; na wana wa Izrahia; Mikaeli, na Obadia, na Yoeli, na Ishia, watano; wote wakuu.

4. Na pamoja nao, katika vizazi vyao, sawasawa na mbari za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu thelathini na sita elfu; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi.

5. Na ndugu zao katika jamaa zote za Isakari, watu hodari wa vita, wakihesabiwa kwa vizazi vyao, walikuwa watu themanini na saba elfu.

6. Wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Yediaeli, watatu.

7. Na wana wa Bela; Esboni, na Uzi, na Uzieli, na Yerimothi, na Iri, watano; wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita; nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao watu ishirini na mbili elfu na thelathini na wanne.

8. Na wana wa Bekeri; Zemira, na Yoashi, na Eliezeri, na Elioenai, na Omri, na Yeremothi, na Abiya, na Anathothi, na Alemethi. Hao wote ndio wana wa Bekeri.

9. Nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao, katika vizazi vyao, wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, jumla yao watu ishirini elfu na mia mbili.

1 Nya. 7