1 Nya. 6:47-67 Swahili Union Version (SUV)

47. mwana wa Mali, mwana wa Mushi, mwana wa Merari, mwana wa Lawi.

48. Na ndugu zao, Walawi, ndio waliowekwa ili kufanya huduma yote ya maskani ya nyumba ya Mungu.

49. Lakini Haruni na wanawe ndio waliokuwa wakitoa sadaka juu ya madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa, na juu ya madhabahu ya kufukizia uvumba, kwa ajili ya kazi yote ya Patakatifu pa Patakatifu, ili kufanya upatanisho kwa Israeli, sawasawa na yote aliyokuwa ameyaamuru Musa, mtumishi wa Mungu.

50. Na hawa ndio wana wa Haruni; mwanawe huyo ni Eleazari, na mwanawe huyo ni Finehasi, na mwanawe huyo ni Abishua;

51. na mwanawe huyo ni Buki, na mwanawe huyo ni Uzi, na mwanawe huyo ni Serahia;

52. na mwanawe huyo ni Merayothi, na mwanawe huyo ni Amaria, na mwanawe huyo Ahitubu;

53. na mwanawe huyo ni Sadoki, na mwanawe huyo ni Ahimaasi.

54. Basi haya ndiyo makao yao, sawasawa na marago yao mipakani mwao; wana wa Haruni, katika jamaa za Wakohathi; kwani walikuwa na kura ya kwanza;

55. wakapewa Hebroni, katika nchi ya Yuda, na vijiji vyake vilivyouzunguka;

56. bali mashamba ya mji huo, na vijiji vyake, alipewa Kalebu, mwana wa Yefune.

57. Na wana wa Haruni wakapewa miji ile ya kukimbilia, nayo ni Hebroni, tena Libna pamoja na viunga vyake, na Yatiri, na Eshtemoa pamoja na viunga vyake;

58. na Holoni pamoja na viunga vyake, na Debiri pamoja na viunga vyake;

59. na Ashani pamoja na viunga vyake, na Beth-shemeshi pamoja na viunga vyake;

60. tena katika kabila ya Benyamini; Geba pamoja na viunga vyake, na Alemethi pamoja na viunga vyake, na Anathothi pamoja na viunga vyake. Miji yao yote katika jamaa zao ilikuwa miji kumi na mitatu.

61. Nao waliobaki wa wana wa Kohathi walipewa kwa kura miji kumi, katika jamaa ya kabila hiyo, yaani, nusu-kabila, nusu ya Manase.

62. Na wana wa Gershoni walipewa kwa kura miji kumi na mitatu, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Isakari, na katika kabila ya Asheri, na katika kabila ya Naftali, na katika kabila ya Manase waliokaa Bashani.

63. Na wana wa Merari walipewa kwa kura miji kumi na miwili, sawasawa na jamaa zao, katika kabila ya Reubeni, na katika kabila ya Gadi, na katika kabila ya Zabuloni.

64. Na wana wa Israeli waliwapa Walawi miji hiyo pamoja na viunga vyake.

65. Tena wakawapa kwa kura miji hiyo iliyotajwa majina yake, katika kabila ya wana wa Yuda, na katika kabila ya wana wa Simeoni, na katika kabila ya wana wa Benyamini.

66. Na jamaa nyingine za wana wa Kohathi walikuwa na miji ya mipakani mwao katika kabila ya Efraimu.

67. Basi wakapewa miji ya kukimbilia, yaani, Shekemu pamoja na viunga vyake katika nchi ya milima milima ya Efraimu; na Gezeri pamoja na viunga vyake;

1 Nya. 6