1 Nya. 4:2-12 Swahili Union Version (SUV)

2. Na Reaya, mwana wa Shobali, akamzaa Yahathi; na Yahathi akawazaa Ahumai, na Lahadi. Hizo ndizo jamaa za Wasorathi.

3. Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na umbu lao aliitwa jina lake Haselelponi;

4. na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrathi, babaye Bethlehemu.

5. Naye Ashuri, babaye Tekoa, alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.

6. Naye Naara akamzalia Ahuzamu, na Heferi, na Temeni, na Ahashtari. Hao ndio wana wa Naara.

7. Na wana wa Hela walikuwa Serethi, na Ishari, na Ethnani.

8. Na Hakosi akawazaa Anubu, na Sobeba, na jamaa za Aharheli, mwana wa Harumu.

9. Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita jina lake Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nalimzaa kwa huzuni.

10. Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibarikia kweli kweli, na kunizidishia hozi yangu, na mkono wako ungekuwa pamoja nami, nawe ungenilinda na uovu, ili usiwe kwa huzuni yangu! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.

11. Naye Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, aliyekuwa babaye Eshtoni.

12. Na Eshtoni akamzaa Beth-Rafa, na Pasea, na Tehina, babaye Ir-nahashi. Hao ni watu wa Reka.

1 Nya. 4