24. Wana wa Uzieli, Mika; wa wana wa Mika, Shamiri.
25. Nduguye Mika, Ishia; wa wana wa Ishia, Zekaria.
26. Wana wa Merari; Mali na Mushi; wana wa Yaazia; Beno.
27. Wana wa Merari; wa Yaazia; Beno, na Shohamu, na Zakuri, na Ibri.
28. Wa Mali; Eleazari, asiyekuwa na wana.
29. Wa Kishi; wana wa Kishi; Yerameeli.
30. Na wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi. Hao ndio wana wa Walawi, kwa kufuata mbari za baba zao.
31. Hao nao wakatupiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa mbari za baba za makuhani na za Walawi; mbari za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.