1 Nya. 24:15-26 Swahili Union Version (SUV)

15. ya kumi na saba Heziri, ya kumi na nane Hapisesi;

16. ya kumi na kenda Pethahia, ya ishirini Ezekieli;

17. ya ishirini na moja Yakini, ya ishirini na mbili Gamuli;

18. ya ishirini na tatu Delaya, ya ishirini na nne Maazia.

19. Huu ndio usimamizi wao katika huduma yao, waingie nyumbani mwa BWANA kwa kadiri ya agizo lao, kwa mkono wa Haruni baba yao, kama BWANA, Mungu wa Israeli, alivyomwamuru.

20. Na wa wana wa Lawi, waliosalia; wa wana wa Amramu, Shebueli; wa wana wa Shebueli, Yedeya.

21. Wa Rehabia; wa wana wa Rehabia, Ishia mkuu wao.

22. Wa Waishari, Shelomothi; wa wana wa Shelomothi, Yahathi.

23. Na wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, Yekameamu wa nne.

24. Wana wa Uzieli, Mika; wa wana wa Mika, Shamiri.

25. Nduguye Mika, Ishia; wa wana wa Ishia, Zekaria.

26. Wana wa Merari; Mali na Mushi; wana wa Yaazia; Beno.

1 Nya. 24