11. Naye Yahathi alikuwa mkubwa wao, na Zina alikuwa wa pili; lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; basi wakawa mbari ya baba kwa kuhesabiwa pamoja.
12. Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne.
13. Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.
14. Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila ya Lawi.
15. Wana wa Musa; Gershomu na Eliezeri.
16. Wana wa Gershomu; Shebueli mkuu wao.
17. Na wana wa Eliezeri; Rehabia mkuu wao. Yeye Eliezeri hakuwa na wana wengine; lakini wana wa Rehabia walikuwa wengi sana.
18. Wana wa Ishari; Shelomithi mkuu wao.
19. Wana wa Hebroni; Yeria mkuu wao, Amaria wa pili, Yahazieli wa tatu, na Yekameamu wa nne.
20. Wana wa Uzieli; Mika mkuu wao, na Ishia wa pili.
21. Wana wa Merari; Mali na Mushi. Wana wa Mali; Eleazari, na Kishi.
22. Akafa Eleazari, wala hakuwa na wana, ila binti tu; na ndugu zao, wana wa Kishi, wakawaoa.
23. Wana wa Mushi; Mali, na Ederi, na Yeremothi, watu watatu.
24. Hao walikuwa wana wa Lawi, kwa kufuata mbari za baba zao, yaani, vichwa vya mbari za baba zao waliohesabiwa, kwa hiyo hesabu ya majina yao kwa vichwa, hao walioifanya kazi ya utumishi wa nyumba ya BWANA, wenye miaka ishirini na zaidi.
25. Kwa kuwa Daudi alisema, BWANA, Mungu wa Israeli, amewastarehesha watu wake; naye hukaa Yerusalemu milele;
26. wala Walawi hawahitaji tena kuichukua maskani, na vyombo vyake vyote kwa utumishi wake.