1 Nya. 23:1-14 Swahili Union Version (SUV)

1. Basi Daudi alikuwa mzee, ameshiba siku; akamtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme juu ya Israeli.

2. Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.

3. Nao wakahesabiwa Walawi wenye miaka thelathini na zaidi; na jumla yao kwa vichwa, mtu kwa mtu, ikapata thelathini na nane elfu.

4. Katika hao ishirini na nne elfu walikuwa wa kusimamia kazi ya nyumba ya BWANA; na sita elfu walikuwa maakida na makadhi;

5. na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu BWANA kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.

6. Basi Daudi akawagawanya kuwa zamu zao sawasawa na wana wa Lawi; Gershoni, Kohathi, na Merari.

7. Wa Wagershoni; Ladani, na Shimei.

8. Wana wa Ladani; Yehieli mkuu wao, na Zethamu, na Yoeli, watu watatu.

9. Wana wa Shimei; Shelomothi, na Hazieli, na Harani, watatu. Hao walikuwa vichwa vya mbari za baba za Ladani.

10. Na wana wa Shimei; Yahathi, na Zina, na Yeushi, na Beria. Hao wanne walikuwa wana wa Shimei.

11. Naye Yahathi alikuwa mkubwa wao, na Zina alikuwa wa pili; lakini Yeushi na Beria hawakuwa na wana wengi; basi wakawa mbari ya baba kwa kuhesabiwa pamoja.

12. Wana wa Kohathi; Amramu, Ishari, Hebroni, na Uzieli, watu wanne.

13. Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.

14. Lakini kwa habari za Musa, mtu wa Mungu, wanawe hutajwa miongoni mwa kabila ya Lawi.

1 Nya. 23