9. Mwimbieni, mwimbieni kwa zaburi;Zitafakarini ajabu zake zote.
10. Jisifuni kwa jina lake takatifu;Na ufurahi moyo wao wamtafutao BWANA.
11. Mtakeni BWANA na nguvu zake;Utafuteni uso wake siku zote.
12. Zikumbukeni ajabu zake alizozifanya;Miujiza yake na hukumu za kinywa chake;
13. Enyi wazao wa Israeli, mtumishi wake,Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
14. Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu;Duniani mwote mna hukumu zake.