1 Nya. 16:29-32 Swahili Union Version (SUV)

29. Mpeni BWANA utukufu wa jina lake;Leteni sadaka, mje mbele zake;Mwabuduni BWANA kwa uzuri wa utakatifu;

30. Tetemekeni mbele zake, nchi yote.Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike;

31. Mbingu na zifurahi, nchi na ishangilie;Na waseme katika mataifa, BWANA ametamalaki;

32. Bahari na ivume na vyote viijazavyo;Mashamba na yashangilie na vyote vilivyomo;

1 Nya. 16