14. Yeye, BWANA, ndiye Mungu wetu;Duniani mwote mna hukumu zake.
15. Likumbukeni agano lake milele,Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
16. Agano alilofanya na Ibrahimu,Na uapo wake kwa Isaka;
17. Alilomthibitishia Yakobo kuwa amri,Na Israeli liwe agano la milele.
18. Akisema, Nitakupa wewe nchi ya Kanaani,Iwe urithi wenu mliopimiwa;
19. Mlipokuwa watu wawezao kuhesabiwa;Naam, watu wachache na wageni ndani yake.
20. Wakatanga-tanga toka taifa hata taifa,Toka ufalme mmoja hata kwa watu wengine.
21. Hakumwacha mtu awaonee;Hata wafalme aliwakemea kwa ajili yao;