1 Nya. 14:8-13 Swahili Union Version (SUV)

8. Na waliposikia hao Wafilisti ya kwamba Daudi ametiwa mafuta ili awe mfalme juu ya Israeli wote, Wafilisti wote wakapanda kumtafuta Daudi; naye Daudi akasikia, akatoka nje kupigana nao.

9. Basi hao Wafilisti walikuwa wamekuja na kuteka nyara katika bonde la Warefai.

10. Daudi akamwuliza Mungu, kusema, Je! Nipande juu ya Wafilisti! Utawatia mikononi mwangu? Naye BWANA akamwambia, Panda; kwa kuwa nitawatia mikononi mwako.

11. Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, BWANA amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu.

12. Nao wakaiacha miungu yao huko; naye Daudi akaamuru, ikateketezwa kwa moto.

13. Lakini hao Wafilisti wakateka nyara tena mara ya pili bondeni.

1 Nya. 14