1 Nya. 11:1-3 Swahili Union Version (SUV)

1. Ndipo Israeli wote wakamkusanyikia Daudi huko Hebroni, wakisema, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako.

2. Katika zamani za kale, hata hapo Sauli alipokuwa mfalme, wewe ndiwe uliyewatoa na kuwaingiza Israeli. Naye BWANA, Mungu wako, akakuambia, Ndiwe, utakayewalisha watu wangu Israeli, ndiwe utakayekuwa mkuu juu ya watu wangu Israeli.

3. Basi wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao huko Hebroni mbele za BWANA; nao wakamtia Daudi mafuta, awe mfalme wa Israeli, sawasawa na neno la BWANA kwa mkono wa Samweli.

1 Nya. 11