Basi wazee wote wa Israeli wakamjia mfalme huko Hebroni; naye Daudi akafanya agano nao huko Hebroni mbele za BWANA; nao wakamtia Daudi mafuta, awe mfalme wa Israeli, sawasawa na neno la BWANA kwa mkono wa Samweli.