1 Nya. 1:37-47 Swahili Union Version (SUV)

37. Wana wa Reueli; Nahathi, na Zera, na Shama, na Miza.

38. Na wana wa Seiri; Lotani, na Shobali, na Sibeoni, na Ana, na Dishoni, na Eseri, na Dishani.

39. Na wana wa Lotani; Hori, na Hemamu; na Timna ni umbu lake Lotani.

40. Wana wa Shobali; Alvani, na Manahathi, na Ebali, na Shefo, na Onamu. Na wana wa Sibeoni; Aya, na Ana.

41. Wana wa Ana; Dishoni. Na wana wa Dishoni; Hemdani, na Eshbani, na Ithrani, na Kerani.

42. Wana wa Eseri; Bilhani, na Zaawani, na Akani. Wana wa Dishani; Usi, na Arani.

43. Basi hawa ndio wafalme waliomiliki katika nchi ya Edomu, kabla hajamiliki mfalme awaye yote juu ya wana wa Israeli; Bela, mwana wa Beori; na jina la mji wake ni Dinhaba.

44. Bela akafa, naye Yobabu, mwana wa Zera, wa Bosra, akamiliki badala yake.

45. Yobabu akafa, naye Hushamu, wa nchi ya Watemani, akamiliki badala yake.

46. Hushamu akafa, naye Hadadi, mwana wa Bedadi, akamiliki badala yake, ambaye aliwapiga Midiani katika uwanja wa Moabu; na jina la mji wake ni Avithi.

47. Hadadi akafa, naye Samla, wa Masreka, akamiliki badala yake.

1 Nya. 1