7. Kwa maana kweli haimpasi mwanamume kufunikwa kichwa, kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume.
8. Maana mwanamume hakutoka katika mwanamke, bali mwanamke katika mwanamume.
9. Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwanamke, bali mwanamke kwa ajili ya mwanamume.
10. Kwa hiyo imempasa mwanamke awe na dalili ya kumilikiwa kichwani, kwa ajili ya malaika.
11. Walakini si mwanamke pasipo mwanamume, wala mwanamume pasipo mwanamke, katika Bwana.
12. Maana kama mwanamke alitoka katika mwanamume, vile vile mwanamume naye huzaliwa na mwanamke; na vitu vyote asili yake hutoka kwa Mungu. Hukumuni ninyi wenyewe katika nafsi zenu.
13. Je! Inapendeza mwanamke amwombe Mungu asipofunikwa kichwa?