1 Fal. 5:13-16 Swahili Union Version (SUV)

13. Mfalme Sulemani akafanya shokoa ya Israeli wote; nayo shokoa hiyo ilikuwa ya watu thelathini elfu.

14. Akawatuma Lebanoni kwa mwezi, elfu kumi kwa zamu. Mwezi mmoja walikuwako huko Lebanoni, na miezi miwili wakawako kwao. Na Adoramu alikuwa juu ya shokoa.

15. Sulemani alikuwa na wachukua mizigo sabini elfu, na wakatao miti themanini elfu milimani;

16. mbali na maakida yake Sulemani waliokuwa juu ya kazi, elfu tatu na mia tatu, wasimamizi wa watu waliotenda kazi.

1 Fal. 5