1 Fal. 4:28-32 Swahili Union Version (SUV)

28. Shayiri pia na majani kwa farasi, na kwa wanyama wenye mbio, wakaleta mahali walipokuwapo, kila mtu kwa kadiri ya kazi yake.

29. Mungu akampa Sulemani hekima, na akili nyingi sana, na moyo mkuu, kama mchanga ulioko pwani.

30. Hekima ya Sulemani ikapita hekima ya wana wote wa mashariki, na hekima zote za Misri.

31. Kwa kuwa alikuwa na hekima kuliko watu wote; kuliko Ethani Mwezrahi, na Hemani, na Kalkoli, na Darda, wana wa Maholi; zikaenea sifa zake kati ya mataifa yote yaliyozunguka.

32. Naye akanena mifano elfu tatu, na nyimbo zake zilikuwa elfu moja na tano.

1 Fal. 4