1 Fal. 18:6-11 Swahili Union Version (SUV)

6. Basi wakaigawanya nchi, ili wapite katika nchi yote; Ahabu akaenda zake njia moja peke yake, na Obadia akaenda zake njia nyingine peke yake.

7. Na Obadia alipokuwa njiani, kumbe! Eliya akakutana naye. Akamtambua, akaanguka kifudifudi, akanena, Je! Ni wewe, bwana wangu Eliya?

8. Akamjibu, Ni mimi. Enenda, umwambie bwana wako, Tazama, Eliya yupo.

9. Akamwambia, Nimekosa nini, hata unitie mimi mtumishi wako mkononi mwa Ahabu, aniue?

10. Kama BWANA, Mungu wako, aishivyo, hakuna taifa wala ufalme ambao bwana wangu hakutuma watu wakutafute; na waliposema, Hayupo, akawaapisha ule ufalme, na taifa, ya kwamba hawakukuona.

11. Nawe sasa wasema, Enenda, umwambie bwana wako, Tazama, Eliya yupo.

1 Fal. 18