1. Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la BWANA, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba.
2. Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la BWANA akasema, Ee madhabahu, madhabahu, BWANA asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.
3. Akatoa ishara siku ile ile, akasema, Hii ndiyo ishara aliyoinena BWANA, Tazama, madhabahu itapasuka, na majivu yaliyo juu yake yatamwagika.
4. Ikawa, mfalme Yeroboamu alipoyasikia maneno ya yule mtu wa Mungu, alipopiga kelele juu ya madhabahu huko Betheli, alinyosha mkono wake pale madhabahuni, akasema, Mkamateni. Basi ule mkono wake aliounyosha ukakatika, wala hakuweza kuurudisha kwake tena.
5. Madhabahu ikapasuka, majivu ya madhabahuni yakamwagika, sawasawa na ishara aliyoitoa mtu wa Mungu kwa neno la BWANA.
6. Mfalme akajibu, akamwambia yule mtu wa Mungu, Umsihi sasa BWANA, Mungu wako, ukaniombee, ili nirudishiwe mkono wangu tena. Yule mtu wa Mungu akamwomba BWANA mkono wa mfalme ukarudishwa tena, ukawa kama ulivyokuwa kwanza.
7. Mfalme akamwambia mtu wa Mungu, Karibu nyumbani kwangu ujiburudishe, nami nitakupa thawabu.
8. Mtu wa Mungu akamwambia mfalme, Ujaponipa nusu ya nyumba yako, sitaingia pamoja nawe, wala sitakula chakula, wala sitakunywa maji mahali hapa;
9. maana ndivyo nilivyoagizwa kwa neno la BWANA, kusema, Usile chakula cho chote wala usinywe maji, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.
10. Basi akaenda zake kwa njia nyingine, wala hakurudi kwa njia ile aliyoijia Betheli.
11. Basi nabii mmoja mzee alikuwa akikaa katika Betheli; na wanawe wakamwendea wakamwambia kila neno alilolitenda yule mtu wa Mungu siku ile katika Betheli; na maneno aliyomwambia mfalme, hayo nayo walimwambia baba yao.
12. Baba yao akawaambia, Amekwenda zake kwa njia ipi? Kwa maana wanawe walikuwa wameiona njia ile aliyoiendea yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda.
13. Akawaambia wanawe, Nitandikieni punda. Wakamtandikia punda, naye akampanda.
14. Akamfuata mtu wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni, akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda? Akamwambia, Mimi ndiye.
15. Akamwambia, Karibu kwangu nyumbani, ule chakula.
16. Naye akamwambia, Siwezi kurudi pamoja nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala sinywi maji pamoja nawe hapa;
17. kwani nimeambiwa kwa neno la BWANA, Usile chakula wala usinywe maji huko, wala usirudi kwa njia ile uliyoijia.
18. Akamwambia, Mimi nami ni nabii kama wewe, na malaika akaniambia kwa neno la BWANA, kusema, Mrudishe pamoja nawe nyumbani kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
19. Basi mtu yule akarudi pamoja naye, akala chakula, akanywa maji nyumbani mwake.
20. Hata ikawa, walipokuwa wameketi mezani, neno la BWANA likamjia nabii yule aliyemrudisha;
21. akamlilia yule mtu wa Mungu aliyetoka katika Yuda, akinena, BWANA asema hivi, Kwa sababu umeiasi kauli ya BWANA, wala hukuishika amri ile aliyokuamuru BWANA, Mungu wako,