Basi mtu huyo akapiga kelele juu ya madhabahu, kwa neno la BWANA akasema, Ee madhabahu, madhabahu, BWANA asema hivi, Angalia, mtoto atazaliwa katika nyumba ya Daudi, jina lake Yosia; na juu yako atawachinja makuhani wa mahali pa juu, wanaofukiza uvumba juu yako, na mifupa ya watu itateketezwa juu yako.