Zaburi 39:9-13 Biblia Habari Njema (BHN)

9. Niko kama bubu, sisemi kitu,kwani wewe ndiwe uliyetenda hayo.

10. Usiniadhibu tena;namalizika kwa mapigo yako.

11. Unapomwadhibu mtu dhambi zake kwa kumkemea,unaharibu kama nondo kile akipendacho.Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!

12. Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu;usikilize kilio changu,usikae kimya ninapolia.Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye,ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote.

13. Uache kunitazama nipate kufurahi kidogo,kabla sijaaga dunia, na kutoweka kabisa.

Zaburi 39