Zaburi 39:5-13 Biblia Habari Njema (BHN)

5. Kumbe umenipimia maisha mafupi sana!Maisha yangu si kitu mbele yako.Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!

6. Kweli, kila mtu anapita kama kivuli;jitihada zake zote ni bure tu;anakusanya mali, asijue atakayeipata!

7. Na sasa, ee Bwana, ninatazamia nini?Tumaini langu ni kwako wewe!

8. Uniokoe katika makosa yangu yote;usikubali wapumbavu wanidhihaki.

9. Niko kama bubu, sisemi kitu,kwani wewe ndiwe uliyetenda hayo.

10. Usiniadhibu tena;namalizika kwa mapigo yako.

11. Unapomwadhibu mtu dhambi zake kwa kumkemea,unaharibu kama nondo kile akipendacho.Hakika, kila binadamu ni kama pumzi tu!

12. Usikie sala yangu, ee Mwenyezi-Mungu;usikilize kilio changu,usikae kimya ninapolia.Maana, mimi ni kama mgeni tu apitaye,ni msafiri kama walivyokuwa wazee wangu wote.

13. Uache kunitazama nipate kufurahi kidogo,kabla sijaaga dunia, na kutoweka kabisa.

Zaburi 39