Zaburi 3 Biblia Habari Njema (BHN)

Kuomba msaada asubuhi

(Zaburi ya Daudi alipomkimbia Absalomu)

1. Ee Mwenyezi-Mungu, tazama walivyo wengi adui zangu,ni wengi mno hao wanaonishambulia.

2. Wengi wanasema juu yangu,“Hatapata msaada kwa Mungu.”

3. Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu u ngao yangu kila upande;kwako napata fahari na ushindi wangu.

4. Nakulilia kwa sauti, ee Mungu,nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu.

5. Nalala na kupata usingizi,naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza.

6. Sitayaogopa maelfu ya watu,wanaonizingira kila upande.

7. Uje ee Mwenyezi-Mungu!Niokoe ee Mungu wangu!Wewe wawavunja mataya maadui zangu wote;wawavunja meno waovu wasinidhuru.

8. Mwenyezi-Mungu ndiwe uokoaye;uwape baraka watu wako.