4. Wanaonekana kama farasi,wanashambulia kama farasi wa vita,
5. Wanaporukaruka kwenye vilele vya milima,wanarindima kama magari ya farasi,wanavuma kama mabua makavu motoni.Wamejipanga kama jeshi kubwatayari kabisa kufanya vita.
6. Wakaribiapo, watu hujaa hofu,nyuso zao zinawaiva.
7. Wanashambulia kama mashujaa wa vita;kuta wanazipanda kama wanajeshi.Wote wanakwenda mbele moja kwa moja,bila hata mmoja wao kubadilisha njia.
8. Hakuna amsukumaye mwenziwe;kila mmoja anafuata mkondo wake.Wanapita kati ya vizuizi vya silaha,wala hakuna kiwezacho kuwazuia.
9. Wanauvamia mji,wanapiga mbio ukutani;wanaziparamia nyumba na kuingia,wanapenya madirishani kama wezi.
10. Nchi inatetemeka mbele yao,mbingu zinatikisika.Jua na mwezi vyatiwa giza,nazo nyota zinaacha kuangaza.
11. Mwenyezi-Mungu anaamuru jeshi lake kwa sauti;askari wake ni wengi mno,wanaomtii hawahesabiki.2Siku ya Mwenyezi-Mungu kweli ni kuu na ya kutisha sana!Nani atakayeweza kuistahimili?