49. Babuloni umesababisha vifo duniani kote;sasa wenyewe utaangamizwa kwa mauaji ya Israeli.
50. “Nyinyi mlinusurika kifo,ondokeni sasa, wala msisitesite!Ingawa mko nchi ya mbali mkumbukeni Mwenyezi-Mungu,ukumbukeni pia mji wa Yerusalemu.
51. Mnasema: ‘Tumeaibishwa na kufadhaishwa;aibu imezifunika nyuso zetu,kwa sababu wageni wameingiakatika sehemu takatifu za nyumba ya Mwenyezi-Mungu.’
52. “Kwa hiyo, wakati unakuja,nasema mimi Mwenyezi-Mungu,ambapo nitaviadhibu vinyago vya Babuloni,na majeruhi watapiga kite katika nchi yake yote.
53. Ingawa Babuloni atapanda mpaka mbinguni,na kuziimarisha ngome zake ndefu,waangamizi watakuja kutoka kwangu kumvamia.2Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
54. “Sikiliza! Kilio kinasikika kutoka Babuloni!Kishindo cha maangamizi makubwakutoka nchi ya Wakaldayo!
55. Maana mimi Mwenyezi-Mungu naiangamiza Babuloni,na kuikomesha kelele yake kubwa.Adui ananguruma kama mawimbi ya maji mengi,sauti ya kishindo chao inaongezeka.
56. Naam, mwangamizi anaijia Babuloni;askari wake wametekwa,pinde zao zimevunjwavunjwa.Mimi Mwenyezi-Mungu ni Mungu mwenye kuadhibu,hakika mimi nitalipiza kisasi kamili.
57. Nitawalewesha wakuu na wenye hekima wake,watawala wake, madiwani na askari wake;watalala usingizi wa milele wasiinuke tena.Nasema mimi mfalme ambaye jina langu ni Mwenyezi-Mungu wa Majeshi.
58. “Mimi Mwenyezi-Mungu wa Majeshi nasema:Ukuta mpana wa Babuloniutabomolewa mpaka chini,na malango yake marefuyatateketezwa kwa moto.Watu wanafanya juhudi za bure,mataifa yanajichosha maana mwisho wao ni motoni!”