Yeremia 50:36-43 Biblia Habari Njema (BHN)

36. Kifo kwa waaguzi,wanachotangaza ni upumbavu tu!Kifo kwa mashujaa wake,ili waangamizwe!

37. Kifo kwa farasi wake na uharibifu kwa magari yake,kifo kwa majeshi yake yote ya kukodiwa,ili wawe na woga kama wanawake!Uharibifu kwa hazina zake zoteili zipate kuporwa.

38. Ukame uyapate majiili yapate kukauka!Maana Babuloni ni nchi ya sanamu za miungu,watu ni wendawazimu juu ya vinyago vyao.

39. “Kwa hiyo wanyama wa porini, mbwamwitu pamoja na mbuni, watakaa Babuloni. Hapatakaliwa kamwe na watu vizazi vyote vijavyo.

40. Kama vile mimi Mwenyezi-Mungu nilivyoiangamiza miji ya Sodoma na Gomora na miji ya jirani, vivyo hivyo hapatakuwa na mtu yeyote atakayeishi humo. Naam, hakuna mtu yeyote atakeyekaa huko. Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.

41. “Tazama! Watu wanakuja kutoka kaskazini;taifa lenye nguvu na wafalme wengiwanajitayarisha kutoka miisho ya dunia.

42. Wameshika pinde zao na mikuki;ni watu wakatili na wasio na huruma.Vishindo vyao ni kama mvumo wa bahari,wamepanda farasi.Wamejipanga tayari kwa vita,dhidi yako wewe Babuloni!

43. Mfalme wa Babuloni amesikia habari zao,nayo mikono yake ikawa kama kamba.Ameshikwa na dhiki na uchungu kama mama anayejifungua.

Yeremia 50