Kwa hiyo simba kutoka msituni atawaua;mbwamwitu kutoka jangwani atawararua.Chui anaivizia miji yao.Kila atokaye humo atararuliwa vipandevipande,kwa sababu dhambi zao ni nyingi,maasi yao ni makubwa.