4. Ndipo nilipowaza:“Hawa ni watu duni hawana akili;hawajui matakwa ya Mwenyezi-Mungu,hawajui Sheria ya Mungu wao.
5. Nitawaendea wakuu niongee nao;bila shaka, wao wanajua matakwa ya Mwenyezi-Mungu;wanajua sheria ya Mungu wao.”Lakini wote waliivunja nira yao.Waliikatilia mbali minyororo yao.
6. Kwa hiyo simba kutoka msituni atawaua;mbwamwitu kutoka jangwani atawararua.Chui anaivizia miji yao.Kila atokaye humo atararuliwa vipandevipande,kwa sababu dhambi zao ni nyingi,maasi yao ni makubwa.
7. Mwenyezi-Mungu anauliza:“Nitawezaje kukusamehe ee Yerusalemu?Watu wako wameniasi;wameapa kwa miungu ya uongo.Nilipowashibisha kwa chakula,wao walifanya uzinzi,wakajumuika majumbani mwa makahaba.