Yeremia 5:2-6 Biblia Habari Njema (BHN)

2. Ingawa wanaapa: “Kama Mwenyezi-Mungu aishivyo”,viapo vyao ni vya uongo.

3. Ee Mwenyezi-Mungu, wewe watafuta daima uaminifu.Umewatwanga, lakini hawakuona uchungu;umewateketeza, lakini walikataa kukosolewa.Wamezifanya nyuso zao kuwa ngumu kuliko mwamba;wamekataa kabisa kurudi kwako.

4. Ndipo nilipowaza:“Hawa ni watu duni hawana akili;hawajui matakwa ya Mwenyezi-Mungu,hawajui Sheria ya Mungu wao.

5. Nitawaendea wakuu niongee nao;bila shaka, wao wanajua matakwa ya Mwenyezi-Mungu;wanajua sheria ya Mungu wao.”Lakini wote waliivunja nira yao.Waliikatilia mbali minyororo yao.

6. Kwa hiyo simba kutoka msituni atawaua;mbwamwitu kutoka jangwani atawararua.Chui anaivizia miji yao.Kila atokaye humo atararuliwa vipandevipande,kwa sababu dhambi zao ni nyingi,maasi yao ni makubwa.

Yeremia 5