19. Humo zitatoka nyimbo za shukranina sauti za wale wanaosherehekea.Nitawaongeza na wala hawatakuwa wachache;nitawafanya waheshimiwe wala hawatadharauliwa.
20. Watoto wao watakuwa kama walivyokuwa zamani,jumuiya yao itaimarika mbele yangu,nami nitawaadhibu wote wanaowakandamiza.
21. Kiongozi wao atakuwa mmoja wao,mtawala wao atatokea miongoni mwao.Nitamleta karibu naye atanikaribia;maana, nani anayethubutu kunikaribia kwa nguvu zake?Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.
22. Nanyi mtakuwa watu wangu,nami nitakuwa Mungu wenu.”