30. “Basi, wewe Yeremia utatabiri maneno haya yote dhidi yao, na kusema hivi:Mwenyezi-Mungu atanguruma kutoka juu,atatoa sauti yake kutoka makao yake matakatifu;atanguruma kwa nguvu dhidi ya watu wake,na kupaza sauti kama wenye kusindika zabibu,dhidi ya wakazi wote wa dunia.
31. Vishindo hivyo vitasikika hadi mwisho wa dunia,maana Mwenyezi-Mungu ana mashtaka dhidi ya mataifa;anawahukumu wanadamu wote,na waovu atawaua kwa upanga!Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
32. Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema:“Tazama, maafa yatalikumba taifa moja baada ya lingine,na tufani itazuka kutoka miisho ya dunia.”
33. Siku hiyo, watakaouawa na Mwenyezi-Mungu watatapakaa kutoka upande mmoja wa dunia hadi mwingine. Hawataombolezewa, hawatakusanywa wala kuzikwa; watabaki kuwa mavi juu ya ardhi.
34. Ombolezeni enyi wachungaji;lieni na kugaagaa majivuni enyi wakuu wa kundi;siku za kuchinjwa kwenu na kutawanywa zimefika;mtauawa kama kondoo madume waliochaguliwa.
35. Wachungaji hawatakuwa na pa kukimbilia,wala wakuu wa kundi hawataweza kutoroka.
36. Sikilizeni kilio cha wachungajina mayowe ya wakuu wa kundi!Mwenyezi-Mungu anayaharibu malisho yao,
37. na makundi yaliyokuwa matulivu yameharibiwakwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.
38. Mwenyezi-Mungu amewaacha watu wake,kama vile simba aachavyo pango lake;nchi yao imekuwa jangwa tupu,kwa sababu ya vita vya wadhalimu,na hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.