1. Mwenyezi-Mungu aliniambia: “Nenda ukanunue gudulia la udongo kwa mfinyanzi. Kisha, wachukue baadhi ya wazee wa watu na baadhi ya makuhani viongozi,
2. halafu uende pamoja nao katika bonde la Mwana wa Hinomu, kwa kupitia lango la Vigae. Ukifika huko, tangaza maneno ninayokuambia.
3. Utasema hivi: Sikilizeni neno la Mwenyezi-Mungu enyi wafalme wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu. Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi: Kweli ninaleta maafa mabaya mahali hapa, hata kila mmoja atakayesikia habari zake, atapigwa na bumbuazi.