12. Lakini wao watasema, ‘Hiyo ni bure tu! Tutafuata mipango yetu wenyewe na kila mmoja wetu atafanya kwa kiburi kadiri ya moyo wake mwovu.’”
13. Basi, Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Yaulize mataifa yote:Nani amewahi kusikia jambo kama hili.Israeli amefanya jambo la kuchukiza mno.
14. Je, majabali ya Lebanoni hukosa theluji?Je, vijito vya maji vya milima yake hukauka?
15. Lakini watu wangu wamenisahau mimi,wanafukizia ubani miungu ya uongo.Wamejikwaa katika njia zao,katika barabara za zamani.Wanapitia vichochoroni badala ya njia kuu.