Yeremia 11:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)

1. Neno lilimjia Yeremia kutoka kwa Mwenyezi-Mungu;

2. “Sikiliza masharti ya agano hili, kisha nenda ukawatangazie watu wa Yuda na wakazi wa Yerusalemu.

3. Utawaambia hivi: Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, asema hivi: Na alaaniwe mtu yeyote asiyejali masharti ya agano hili.

Yeremia 11