16. Siku hiyo ni ya mlio wa tarumbeta ya vita,dhidi ya miji yenye ngome na kuta ndefu.
17. Kwa kuwa watu wamemkosea Mwenyezi-Mungu,yeye atawaletea dhiki kubwa,hivyo kwamba watatembea kama vipofu.Damu yao itamwagwa kama vumbi,na miili yao kama mavi.
18. Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoakatika siku hiyo ya ghadhabu ya Mwenyezi-Mungu.Kwa moto wa wivu wakedunia yote itateketezwa.Kwa ukamilifu na kwa namna ya kutishaatawafanya wakazi wote duniani watoweke.