Nahumu 3:7-13 Biblia Habari Njema (BHN)

7. Kisha wote watakaokuona watakukimbia wakisema,“Ninewi umeangamizwa,ni nani atakayeuombolezea?Nani atakayekufariji?”

8. Je, wewe Ninewi, ni bora kuliko Thebesi,mji uliojengwa kando ya mto Nili?Thebesi ulizungukwa na maji,bahari ilikuwa boma lake,maji yalikuwa ukuta wake!

9. Kushi ilikuwa nguvu yake;nayo Misri pia, tena bila kikomo;watu wa Puti na Libia waliusaidia!

10. Hata hivyo, ulichukuliwa mateka,watu wake wakapelekwa uhamishoni.Hata watoto wake walipondwapondwakatika pembe ya kila barabara;watu wake mashuhuri walinadiwa,wakuu wake wote walifungwa minyororo.

11. Ninewi, nawe pia utalewa;utamkimbia adui na kujaribu kujificha.

12. Ngome zako zote ni za tini za mwanzo;zikitikiswa zinamwangukia mlaji kinywani.

13. Tazama askari wako:Wao ni waoga kama wanawake.Milango ya nchi yako ni wazi mbele ya adui zako;moto umeyateketeza kabisa makomeo yake.

Nahumu 3