Kutoka 8:4-7 Biblia Habari Njema (BHN)

4. Vyura watapanda juu ya mwili wako, miili ya watu wako na watumishi wenu!”

5. Mwenyezi-Mungu akamwambia Mose, “Mwambie Aroni anyoshe mkono wake na fimbo yake juu ya mito, juu ya mifereji na madimbwi, nao vyura watatokea na kuenea kila mahali nchini Misri.”

6. Basi, Aroni akanyosha fimbo yake juu ya maji yote, vyura wakatokea na kuifunika nchi nzima ya Misri.

7. Lakini wachawi wa Misri kwa uchawi wao pia wakaleta vyura nchini Misri.

Kutoka 8