Kumbukumbu La Sheria 10:19-22 Biblia Habari Njema (BHN)

19. Basi, wapendeni wageni kwa kuwa nanyi pia mlikuwa wageni nchini Misri.

20. Mcheni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; mtumikieni; ambataneni naye na kuapa kwa jina lake.

21. Yeye ni fahari yenu; ndiye Mungu wenu ambaye amewatendea haya mambo makubwa na ya kutisha mliyoyaona kwa macho yenu wenyewe.

22. Babu zenu walipokwenda Misri, walikuwa watu sabini tu, lakini sasa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewafanya kuwa wengi kama nyota za mbinguni.

Kumbukumbu La Sheria 10