17. Niliwakasirikia kwa sababu ya uovu na tamaa zao;niliwaadhibu, nikauficha uso wangu na kukasirika.Lakini wao waliendelea kufuata njia zao wenyewe.
18. Niliiona mienendo yao, lakini nitawaponya;nitawaongoza na kuwapa faraja,nitawatuliza hao wanaoomboleza.
19. Mimi nitawapa amani,amani kwa walio mbali na walio karibu!Mimi nitawaponya.
20. Lakini waovu ni kama bahari iliyochafuka,ambayo haiwezi kutulia;mawimbi yake hutupa tope na takataka.”
21. Mungu wangu asema hivi:“Watu waovu sitawapa amani.”