7. Alidhulumiwa na kuteswa,lakini alivumilia kwa unyenyekevu,bila kutoa sauti hata kidogo.Alikuwa kama mwanakondoo apelekwaye machinjoni,kama kondoo akaavyo kimya anapokatwa manyoya.Hakutoa sauti hata kidogo.
8. Alidhulumiwa, akahukumiwa na kupelekwa kuuawa;na hakuna mtu aliyejali yanayompata.Alifukuzwa kutoka nchi ya walio hai,kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
9. Walimzika pamoja na wahalifu;katika kifo aliwekwa pamoja na matajiri,ingawa hakutenda ukatili wowote,wala hakusema neno lolote la udanganyifu.
10. Mwenyezi-Mungu alipenda kumwumizana kumweka katika huzuni.Alijitoa mhanga kwa ajili ya kuondoa dhambi.Mtumishi wa Mungu atakuwa na wazawa;ataishi maisha marefu.Yeye ndiye atakayetimiza mpango wa Mwenyezi-Mungu.
11. Mungu asema:“Baada ya kutaabika sana,mtumishi wangu atafurahi.Kwa kuwajibika kwake kikamilifu,atatosheka na matokeo hayo.Kwa maarifa yake mtumishi wangu mwadilifuatawafanya wengi wawe waadilifuYeye atazibeba dhambi zao.