Isaya 49:14-18 Biblia Habari Njema (BHN)

14. Wewe Siyoni wasema:“Mwenyezi-Mungu ameniacha;hakika Bwana wangu amenisahau.”

15. Lakini Mwenyezi-Mungu asema:“Je, mama aweza kumsahau mwanawe anayenyonya,asimwonee huruma mtoto wa tumbo lake?Hata kama mama aweza kumsahau mwanawe,mimi kamwe sitakusahau.

16. Nimekuchora katika viganja vyangu;kuta zako naziona daima mbele yangu.

17. Watakaokujenga upya wanakuja haraka,wale waliokuharibu wanaondoka.

18. Inua macho uangalie pande zote;watu wako wote wanakusanyika na kukujia.Naapa kwa nafsi yangu mimi Mwenyezi-Mungu,watu wako watakuwa kwako kama mapambo,utawafurahia kama afanyavyo bibi arusi na utaji wake.

Isaya 49