Isaya 4:3-6 Biblia Habari Njema (BHN)

3. Wale watakaosalia hai mjini Yerusalemu, naam, wale watakaobaki huko Siyoni, wataitwa “Wateule wa Mungu;” hao ndio wale wote watakaokuwa wameandikwa kitabuni mwake waishi huko Yerusalemu.

4. Kwa roho yake, Bwana atawaweka sawa na kuwatakasa. Na atakapokwisha kuwatakasa wanawake wa Siyoni uchafu wao na kufuta madoa ya damu yaliyomo humo Yerusalemu,

5. hapo atafanya kila mahali juu ya mlima Siyoni na juu ya mikutano ya watu kuwe na wingu wakati wa mchana, na moshi na moto uwakao vizuri wakati wa usiku. Zaidi ya hayo utukufu wa Mungu utaufunika na kuulinda mji wote.

6. Utukufu wake utakuwa kwao kivuli kuwakinga na joto la mchana; na kimbilio na kinga yao wakati wa dhoruba na mvua.

Isaya 4